UWARIDI WAZINDUA WA ANZISHA APP YA KUSOMA RIWAYA MTANDAONI
3/02/2017 12:28:00 am

Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI) wakishirikiana na kampuni ya Dau Technology Limited leo hii wamezindua mfumo maalumu wa kuuza,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu,yani mobile phone application iitwayo “UWARIDI APP”ikiwa na lengo la kukuza utamaduni wa watanzania kupenda kusoma riwaya.

Akizungumza na waandishi wa habari Jiji Dar es salaam Katibu Mkuu wa UWARIDI APP Ibrahim Gama amesema kupitia mfumo huo utaweza kuwasaidia na kuwakomboa waandishi wa riwaya hapa nchini kupata malipo yao muafaka kupitia kazi zao.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *